Kuhusu Kalenda ya Kiuchumi
Kalenda ya Kiuchumi ni kipengele kinachosaidia traders kufuatilia na kuchanganua matukio ya soko, na kubashiri mienendo zaidi ya bei. Inaangazia habari zijazo za kitaifa na kimataifa kote ulimwenguni kwa mpangilio kulingana na tarehe.
Matukio haya makuu yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye masoko ya fedha na kwa kawaida hutangazwa au kutolewa katika ripoti. Mifano ya matukio kama haya ni pamoja na maamuzi ya sera za fedha, indicators za kiuchumi, matangazo ya Pato la Taifa (GDP), nambari za Malipo ya Mashirika Yasiyo ya Kilimo (NFP), maamuzi ya viwango vya riba na mengine mengi.
Traders wa Exness hujulishwa dakika 45 kabla ya wasilisho la taarifa za habari ili kuwajulisha kuhusu wakati na instruments ambazo zitaathiriwa na habari hizo. Arifa hutumwa kupitia barua pepe kwa kichupo cha 'Mailbox' kwenye jukwaa lao la kutrade.